Wapenda urahisi wa manunuzi kwenye mtandao lakini una wasiwasi kuhusu wizi wa utambulisho? Firefox ina vitendakazi vya kuwezesha kuweka habari yako salama. Kwa kufuata mashauri haya rahisi, utapata uzoefu salama na bila ya matatizo.
Kidokezo 1: Nunua tu kutoka maeneo yanayoaminiwa na salama
Angalia kwa kufuli alama juu ya baa ya anwani kabla ya kuwasilisha habari yoyote ya binafsi. Kufuli inaonyesha kwamba uhusiano wako ni salama, hivyo wezi wa utambulisho hawezi "kusikiliza" na kutafuta habari zako za binafsi
Kubofya kwenye icon kwenye baa ya anwani yako pia itakuambia ambaye anamiliki tovuti na ambaye alithibitisha. Habari hii husaidia kuepuka maeneo bandia ambayo hujaribu kukuhadaa kuwapa habari yako.
Kwa habari zaidi, angalia unavoweza kujua ikiwa uhusiano wangu na tovuti ni salama
Kidokezo 2: Tumia manenosiri thabiti
Epuka kujenga manenosiri ambayo ni rahisi kubahatisha, na jaribu kutumia nywila tofauti katika akaunti zako zote mtandaoni. Fuata vidokezo hivi ili kuweka manenosiri thabiti ambazo ni rahisi kwako wewe kukumbuka, lakini ni vigumu kwa wengine kutambua.
Kidokezo 3: Linda habari yako ya kuvinjari
Wakati unashiriki kompyuta yako na wengine, fuata vidokezo hizi kuweka habari yako, kama vile historia ya kuvinjari na logins, binafsi:
- Tumia Private Browsing mode wakati wa ununuzi ili kuzuia historia, mapendeleo yako ya tovuti au logins kuhifadhiwa na kupatikana kwa wengine. Private Browsing huzuia kuki kuzuia wadanganyifu na snoops zisifuatilie mwenendo wako.
- Kama ukisahau kutumia hali ya Private Browsing katika kompyuta inayotumiwa na watu wengi, usiwe na wasiwasi. Bado unaweza kutumia kifungo cha kusahau haraka kufuta taarifa yako ya hivi karibuni bila kuathiri wengine.
- Tumia Master Password kulinda habari yako ya kuingia iliyohifadhiwa. Hii inazuia watu wengine kutokana na kutumia taarifa yako iliyohifadhiwaza kuingia kwa akaunti yako au kifaa kilichoibiwa.